Moto wafika kwenye moyo wa utawala wa Kizayuni; kambi ya jeshi na makumbusho vyateketea
(last modified Thu, 01 May 2025 05:27:03 GMT )
May 01, 2025 05:27 UTC
  • Moto wafika kwenye moyo wa utawala wa Kizayuni; kambi ya jeshi na makumbusho vyateketea

Moto mkubwa unaendelea kuteketeza maeneo mengi ya utawala ghasibu wa Israel huku opereshei ya kuhamisha wakazi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ikiendelea. Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeiripoti kuwa moto huo umeenea katika maeneo mapya ya Quds inayokaliwa kwa mabavu (Jerusalem ) na kusambaa hadi katika makumbusho ya zana za kivita za jeshi la Israel.

Vyombo vya habari vya Israel vimeonyesha mkanda wa video wa moto huo ukisambaa kwa kasi kubwa na kuripoti kuwa umefika kwenye jumba la makumbusho la zana za kivita za Israel huko Latrun, lililoko karibu na Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.

Moto ukiteketeza makumbusho ya zana za kivita ya Israel

Baadhi ya vyombo vya habari pia vimeripoti kuwa moto huo umesambaa hadi katika mji wa Afula ulioko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopachikwa jina la Israel.

Televisheni ya Israel imeripoti kuwa Italia na Ugiriki ni miongoni mwa nchi za kwanza kuitikia ombi la msaada kwa ajili ya kudhibiti moto huo.

Watu watatu wametiwa mbaroni hadi sasa kwa tuhuma za kuhusika na moto huo.

Hata hivyo, Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel mwenye misismamo ya kibaguzi, Itamar Ben-Gvir amedai kuwa moto huo umesababishwa na Wapalestina na kusema wanapaswa kunyongwa!