Jeshi la utawala wa Kizayuni lakiri kuwa askari wake wawili wameangamizwa Ghaza
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limekiri kuwa wanajeshi wake wawili wameuawa katika Ukanda wa Ghaza.
Taarifa ya Al-Qassam imesema, wapiganaji wake waliwashambulia wanajeshi saba wa Israel kwa mada zenye miripuko mikubwa karibu na Msikiti wa Omar ibn Abd al-Aziz katika kitongoji cha al-Tannour mashariki mwa Rafah.
Brigedi za Al-Qassam ziliripoti hapo awali kwamba zililenga kitengo cha uhandisi cha Israel cha wanajeshi 12 kilichokuwa kikijiandaa kutekeleza operesheni ya ubomoaji ndani ya nyumba karibu na makutano ya al-Fidai katika kitongoji hicho.
Taarifa ya Al-Qassam imesema, mripuko uliotokea ndani ya nyumba hiyo ulisababisha vifo vingi, na kwamba brigedi hizo ziliona helikopta za Israel zikitua eneo la tukio kuwaondoa maiti na majeruhi.../