Mufti wa Oman: Wayameni wamevunja kila ngano na wamewafukuza maadui
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128958-mufti_wa_oman_wayameni_wamevunja_kila_ngano_na_wamewafukuza_maadui
Mufti wa Oman ametoa tena pongezi zake kwa taifa la Yemen na kubainisha kwamba, walivunja kila ngano na wakawafukuza maadui.
(last modified 2025-07-31T00:45:39+00:00 )
Jul 31, 2025 00:45 UTC
  • Mufti wa Oman: Wayameni wamevunja kila ngano na wamewafukuza maadui

Mufti wa Oman ametoa tena pongezi zake kwa taifa la Yemen na kubainisha kwamba, walivunja kila ngano na wakawafukuza maadui.

Mufti wa Oman, Sheikh Ahmed Al-Khalili, amerejelea shukrani na sifa zake kwa misimamo ya uungaji mkono ya Yemen kwa wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya mauaji ya halaiki, mzingiro, njaa na kunyimwa haki na adui wa Israel kwa takriban miaka miwili.

Sheikh Al-Khalili amesema: “Mwenyezi Mungu awabariki mashujaa wa Yemen, ambao ni simba wakali wasioweza kushindwa, Mungu awazidishie uthabiti, uimara, nguvu na ushujaa, na awajaalie ushindi wa wazi.

Hivi karibuni pia Mufti Mkuu Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili, alisisitiza kuwa, leo hii majeshi ya madola dhalimu na ya kibeberu duniani yameinamisha vichwa vyao mbele ya Yemen na akayataka mataifa yanayotaka kuwa huru duniani, kuiga mfano wa Yemen katika kukabiliana na maadui wa mataifa yao.

Mufti wa Oman aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Kuna mafunzo na maadili makubwa tuliyoyaona… Mambo ya kufurahisha tuliyoyashuhudia huko Yemen ni mengi… linatutosha somo tulilopata kutokana na kusimamia kwao imara kukabiliana na dola kubwa la dhulma na na la kibeberu (Marekani) na kulilazimisha kusalimu amri na kurudi nyuma.

Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed al-Khalili, amewahi pia kukosoa vikali mara kadhaa kimya kinachoonyeshwa mbele ya jinai za kinyama zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.