Watoto 20,000 wa Gaza wanatabika kwa utapiamlo mkali
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129034-watoto_20_000_wa_gaza_wanatabika_kwa_utapiamlo_mkali
 Shirika la kimataifa la "Action Against Hunger" limeonya kwamba mzozo wa njaa katika Ukanda wa Gaza umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na hilo limekuwa matokeo ya kimajanga kwa watoto na wanawake wa Ukanda huo.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Aug 01, 2025 23:09 UTC
  • Watoto 20,000 wa Gaza wanatabika kwa utapiamlo mkali

 Shirika la kimataifa la "Action Against Hunger" limeonya kwamba mzozo wa njaa katika Ukanda wa Gaza umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na hilo limekuwa matokeo ya kimajanga kwa watoto na wanawake wa Ukanda huo.

Kulingana na shirika hilo, kwa akali watoto 20,000 wamehamishiwa katika hospitali za Gaza kutokana na utapiamlo mkali, na hali ya afya ya umma ni mbaya sana. Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa watoto 300,000 walio chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha 150,000 wanahitaji sana virutubisho vya haraka vya lishe.

Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNPF) umewahi kutahadharisha kuhusu taathira hasi za utapiamlo zinazowakodolea macho wanawake wajawazito na watoto wachanga katika Ukanda wa Gaza; huku vita vya kikatili na vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo vikishadidi.

Wakati huo huo, maafisa wa utoaji misaada katika Ukanda wa Ghaza wametangaza kuwa, zaidi ya watu 127 wamekufa shahidi kwa utapiamlo na njaa kutokana na mzingiro mkubwa lililowekewa eneo hilo na utawala wa kizayuni na hatua ya utawala huo ghasibu ya kuzuia uingizaji misaada ya kibinadamu.

Huku jinai za utawala wa kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza zikiwa zinaendelea, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika eneo hilo lililozingirwa na linalokabiliwa na vita vya kinyama tangu baada ya kutekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba 2023 imepindukia 60,000.