Waandishi wa habari 195 wametiwa mbaroni Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129256-waandishi_wa_habari_195_wametiwa_mbaroni_palestina
Waandishi habari wasiopungua 195 wameripotiwa kutiwa mbaroni na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina tangu kujiri Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa iliyopelekezwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
(last modified 2025-08-07T08:26:52+00:00 )
Aug 07, 2025 08:26 UTC
  • Waandishi wa habari 195 wametiwa mbaroni Palestina

Waandishi habari wasiopungua 195 wameripotiwa kutiwa mbaroni na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina tangu kujiri Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa iliyopelekezwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Klabu ya Wafungwa wa Palestina imetangaza kuwa, tangu kuanza vita vya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, utawala wa Israel umewatia mbaroni waandishi 195 katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Waandishi 55 kati ya hawa bado wako kizuizini. Hapo awali, Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina ilitangaza kuwa waandishi wa habari 232 wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita hivyo.

Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari nchini Marekani sambamba na kutangaza kuwa, idadi kubwa ya waandishi wa habari waliuawa duniani kote mwaka jana imeeleza kwamba, utawala wa Kizayuni umehusika na mauaji ya takriban asilimia 70 ya waandishi hao.

Waandishi wa habari ni miongoni mwa wahanga wakuu wa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza.

Waandishi wa habari ni miongoni mwa wahanga wakuu wa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza. Jinai iliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita dhidi ya Gaza haikuwa na mfano wake katika vita vya miongo ya hivi karibuni.

Wakati wa uvamizi wa Marekani dhidi ya Vietnam, ambao ulidumu kwa karibu miaka 20, waandishi wa habari 63 waliuawa, na waandishi wa habari 17 waliuawa katika Vita vya Peninsula ya Korea katika vilivyodumu kwa muda wa miaka 3. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa, Gaza lilikuwa eneo hatari zaidi duniani mwaka jana. Waandishi wa habari waliuawa na utawala wa Kizayuni kwa sababu tu walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi, yaani kuakisi na kuripoti habari za matukio ya vita vya Gaza.