Idadi ya wanaokufa kwa lisheduni Gaza inazidi kuongezeka
Idadi ya watu wanaokufa kwa lisheduni katika Ukanda wa Gaza huko Gaza inazidi kuongezeka.
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza ilmetangaza kuwa, watu wanne zaidi wamefariki dunia kutokana na njaa na utapiamlo katika muda wa saa 24 zilizopita.
Kwa hesabu hii, jumla ya mashahidi wa njaa na utapiamlo katika Ukanda wa Gaza imefikia 239, kati yao 106 ni watoto, imeeleza taarifa hiyo ya Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza.
Maafisa wa utoaji misaada katika Ukanda wa Ghaza wamebainisha kuwa, watu zaidi ya 200 wamekufa shahidi kwa utapiamlo na njaa kutokana na mzingiro mkubwa lililowekewa eneo hilo na utawala wa kizayuni na hatua ya utawala huo ghasibu ya kuzuia uingizaji misaada ya kibinadamu.
Shirika la kimataifa la "Save the Children" limetangaza kuwa, mzingiro wa Israel umewaweka watoto katika Gaza kwenye njaa mbaya, na hadi sasa watoto 100 wamekufa kutokana na njaa.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema: Zaidi ya watu 500,000, robo ya wakazi wa Gaza, wanakabiliwa na njaa, wakati wengine waliobaki wanakumbana na viwango tofauti vya njaa. Wameongeza kuwa watoto 320,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wa Ukanda wa Gaza wako katika hatari ya utapiamlo mkali.
Huku jinai za utawala wa kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza zikiwa zinaendelea, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika eneo hilo lililozingirwa na linalokabiliwa na vita vya kinyama tangu baada ya kutekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba 2023 imepindukia 61,000.