Mataifa ya Kiislamu yalaani kauli ya Netanyahu ya 'Israel Kubwa Zaidi'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129602-mataifa_ya_kiislamu_yalaani_kauli_ya_netanyahu_ya_'israel_kubwa_zaidi'
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi 31 za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na mashirika ya kieneo, wamelaani vikali matamshi ya Netanyahu kuhusu "Israel Kubwa Zaidi," na kuyataja kuwa ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kitaifa wa Kiarabu na amani ya kikanda.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Aug 16, 2025 04:49 UTC
  • Bendera za baadhi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu zilizotoa taarifa ya kulaani matamshi ya Netanyahu
    Bendera za baadhi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu zilizotoa taarifa ya kulaani matamshi ya Netanyahu

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi 31 za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na mashirika ya kieneo, wamelaani vikali matamshi ya Netanyahu kuhusu "Israel Kubwa Zaidi," na kuyataja kuwa ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kitaifa wa Kiarabu na amani ya kikanda.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi 31 za Kiarabu na Kiislamu, zikiwemo Jordan, Algeria, Bahrain, Bangladesh, Chad, Comoro, Djibouti, Misri, Gambia, Indonesia, Iraq, Kuwait, Lebanon, Libya, Maldives, Mauritania, Morocco, Nigeria, Oman, Pakistan, Palestina, Qatar, Saudi Arabia, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Imarati, Yemen na Uturuki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba, katika taarifa yao ya pamoja, wamelaani vikali matamshi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu "Israel Kubwa Zaidi."

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, matamshi hayo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kanuni za uhusiano wa kimataifa, tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kitaifa wa Kiarabu na mamlaka ya nchi na ni tishio kwa usalama na amani ya kieneo na kimataifa.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ambaye matamshi yake ya mpango wa Israel Kubwa Zaidi yameendelea kulaaniwa kila kona ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu

 

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi  za Kiarabu na Kiislamu sambamba na kusisitiza kuheshimu kwao sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa hususan Kifungu cha 2, ibara ya 4 kuhusu marufuku ya kutumia nguvu au vitisho wametangaza kwamba, nchi hizo zitatekeleza sera na hatua zote zinazohitajika ili kuweka amani, usalama na maendeleo, bila ya aina yoyote ya utawala na mabavu.

Netanyahu alisema hivi majuzi katika mahojiano na chaneli ya i24 News ya Israel: "Ninatekeleza misheni ya kihistoria na ya kiroho na ninashikamana kihisia na ndoto ya Israeli Kubwa Zaidi."

Kauli hiyo ya Netanyahu imeshambuliwa na kulaaniwa vikali na watumiaji wengi wa Kiarabu kwenye mitandao ya kijamii.