Watoto wangapi wanapoteza maisha kila siku huko Gaza?
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza vifo vya kila siku vinavyowakumba wataoto wa Ukanda wa Gaza.
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi Agosti 19 mwaka huu, Wapalestina 62,064 wameuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi na vita vya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza.
Ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina inasema: Idadi jumla ya majeruhi wa mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia 156,573.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza katika ripoti yake kuwa watoto 28 wanauawa shahidi kila siku huko Gaza, na ndio kundi linaloteseka zaidi kwa vita na njaa.
Utawala wa Israel unatumia njaa kama wenzo wa mashinikizo katika mazungumzo yake na wanamapambano wa Kipalestina.
UNRWA imesisitiza kuwa vitisho vya Israel vya kutaka kuikalia kwa mabavu Gaza vitapelekea kuuliwa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya watu na kutatiza zaidi hali ya mambo ya eneo hilo.