Yemen: Tutaendelea kuitia adabu Israel kama haitoheshimu usimamishaji vita Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i131856-yemen_tutaendelea_kuitia_adabu_israel_kama_haitoheshimu_usimamishaji_vita_ghaza
Mamia ya maelfu ya wananchi wa Yemen walifanya mikutano na maandamano ya nchi nzima kitaifa jana wakielezea kuwa kwao tayari kuendelea kuitandika na kuitia adabu Israel kama haitoheshimu makubaliano ya kusitisha vita na kukomesha jinai zake huko Ghaza.
(last modified 2025-10-11T08:57:00+00:00 )
Oct 11, 2025 05:36 UTC
  • Yemen: Tutaendelea kuitia adabu Israel kama haitoheshimu usimamishaji vita Ghaza

Mamia ya maelfu ya wananchi wa Yemen walifanya mikutano na maandamano ya nchi nzima kitaifa jana wakielezea kuwa kwao tayari kuendelea kuitandika na kuitia adabu Israel kama haitoheshimu makubaliano ya kusitisha vita na kukomesha jinai zake huko Ghaza.

Maandamano makubwa ya jana nchini Yemen yamefanyika sambamba na kuanza utekelezaji wa kusimamisha vita katika Ukanda wa Ghaza na kuupongeza Muqawama na hasa wa wananchi wa Ghaza kwa kusimama kidete kujihami na kulinda ardhi yao.

Mikusanyiko ya watu wengi ilifanyika kwenye maeneo mbalimbali ya Yemen, ikiwa ni pamoja na katika mkoa wa Sa’ada kaskazini mwa Yemen, chini ya kaulimbiu inayosema: "Kimbunga cha al Aqsa: Miaka Miwili ya Jihadi na Kujitolea Hadi Ushindi."

Waandamanaji hao wamesisitiza kuwa hawaziamini ahadi zinazotolewa na utawala ghasibu wa Israel na wametangaza kuwa, makubaliano yoyote na utawala huo dhalimu hayaondoi haja ya kuendelea kujitayarisha kwa vita, kitaifa.

Wameongeza kuwa, adui Mzayuni hana historia ya kuheshimu ahadi zake na anaweza kuamua kukwamisha au kufanya ujanja na hila za kishetani za kuvuruga makubaliano ya kusimamisha vita huko Ghaza. Ndio maana wamesisitiza kuwa, watu lazima wawe macho na kutumia kila fursa ili kuendelea kujiweka tayari kwa mazoezi ya kivitendo.

Katika taarifa yao rasmi, waandamanaji hao wa Yemen wamesema kuwa Muqawama wa Palestina kwa uungaji mkono wa wananchi wa Yemen na mataifa ya Kiislamu umefelisha njama zote za Israel na Marekani za kulikandamiza taifa la Palestina na kuuvunja Muqawama wake.

Wananchi wa Yemen aidha wamewashukuru wale wote waliojitolea mhanga kwa ajili ya kuiunga mkono Ghaza, hususan harakati ya Muqawama ya Lebanon ya Hizbullah, Iran na Muqawama wa Iraq.