Ma'ariv: Maafisa 50 wa utawala unaotaka kujitenga Somaliland wamepewa nafunzo Israel
Gazeti la Kiebrania la Ma'ariv limefichua kashfa mpya kuhusu uhusiano wa siri kati ya Tel Aviv na eneo linalotaka kujitenga huko kaskazini mwa Somalia, likiandika kwamba askari 50 wa "Somaliland" wamerejea Afrika baada ya kukamilisha kozi za mafunzo katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).
Kufuatia kuchapishwa habari kwamba eneo la Somaliland linalotaka kujitenga linakusudia kufungua ubalozi huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, gazeti la Israel la Ma'ariv sasa limefichua kwamba, wanajeshi 50 wa eneo la Somaliland wamerejea Afrika baada ya kukamilisha mafunzo yao huko Tel Aviv.
Katika miezi ya hivi karibuni, Israel, katika hatua inayokiuka sheria za kimataifa, imeitambua Somaliland, ambayo inatambuliwa kuwa sehemu ya Somalia, na kumteua balozi wake katika eneo hilo. Somaliland pia wiki iliyopita ilitangaza kufunguliwa ubalozi wake huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.
Nafasi muhimu ya kijiografia ya Somaliland na ukuruba wake kwa Yemen ni mojawapo ya sababu muhimu zaidi za kuvutiwa utawala wa Kizayuni na eneo hilo, ambalo halitambuliwi na jamii ya kimataifa kama nchi inayojitawala, na Israel ndio utawala pekee ambao umetambua rasmi Somaliland na kuteua balozi kwa ajili ya eneo hilo la Somalia.
Gazeti la London, Daily Telegraph, limechapisha ripoti kuhusu harakati za Israel huko Somaliland na kuandika kwamba ujumbe wa Israel ulimpa mkuu wa eneo hilo linalotaka kujitenga na Somalia kipande cha Iron Dome wakati wa sherehe rasmi zilizofanyika katika makao makuu ya eneo hilo, Hargeisa.
Hapo awali, maafisa wa Somaliland walikuwa walipendekeza kwa Tel Aviv kwamba wako tayari kuwapokea Wapalestina wanaofukuzwa na Israel kutoka Gaza katika eneo hilo mkabala wa kutambuliwa rasmi eneo hilo kama nchi huru inayojitawala.