Hizbullah yashambulia vikosi vamizi vya Israel kusini mwa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i138912-hizbullah_yashambulia_vikosi_vamizi_vya_israel_kusini_mwa_lebanon
Wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wametekeleza wimbi la mashambulizi yaliyoratibiwa siku ya Alhamisi, wakilenga ngome kadhaa za kijeshi za Israel na kusababisha hasara kubwa kwa wanajeshi hao vamizi wa Kizayuni.
(last modified 2026-06-05T12:58:14+00:00 )
Jun 05, 2026 11:19 UTC
  • Hizbullah yashambulia vikosi vamizi vya Israel kusini mwa Lebanon

Wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wametekeleza wimbi la mashambulizi yaliyoratibiwa siku ya Alhamisi, wakilenga ngome kadhaa za kijeshi za Israel na kusababisha hasara kubwa kwa wanajeshi hao vamizi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na harakati hiyo ya Muqawama Ijumaa asubuhi, wapiganaji wake walilenga mikusanyiko ya wanajeshi wa Israel pamoja na magari ya kivita katika miji kadhaa ya mpakani ikiwemo Yohmor alShaqif, Rashaf, alQantara na Khiam.

Operesheni hizo zimehusisha mashambulizi makali ya makombora pamoja na ndege zisizo na rubani ambazo zimeshambulia maeneo yaliyokuwa na wanajeshi wa Israel na zana zao za kijeshi.

Eneo la kihistoria linalozunguka Ngome ya Beaufort limeshuhudia mapigano makali zaidi, ambapo wapiganaji wa Hizbullah wameshambulia vituo vya kamandi vya Israel na mikusanyiko ya wanajeshi kwa mawimbi ya mizinga, makombora mazito na mashambulizi sahihi ya ndege zisizo na rubani.

Hizbullah pia imeripoti kuharibiwa vifaru kadhaa vya kisasa aina ya Merkava katika mashambulizi hayo.

Operesheni za Hizbullah zinakuja kama sehemu ya uungaji mkono wake thabiti kwa watu wa Palestina na pia kama jibu la moja kwa moja kwa uchokozi unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni pamoja na majaribio yake ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon.

Muqawama wa Kiislamu, yaani Hizbullah, umeahidi kuilinda mamlaka na uhuru wa Lebanon na kuwasukuma nyuma wanajeshi vamizi wa Israel.

Opereshen za hivi karibuni zinaonyesha kuongezeka ufanisi wa Mhimili wa Muqawama katika kukabiliana na utawala wa Tel Aviv katika nyanja mbalimbali, na kutoa kipigo kikali kwa jeshi la uvamizi licha ya kuwa na silaha za hali ya juu na nguvu kubwa ya anga.

Vikosi vamizi vya Israel vimekabiliwa na ongezeko la vifo na uharibifu wa zana za kijeshi kusini mwa Lebanon huku Hizbullah ikiendelea kuongeza mashinikizo kwa lengo la kuonyesha mshikamano wake na Wapalestina wa Gaza na mapambano mapana ya kikanda dhidi ya sera za kivamizi na kujitanua za Israel.