Mamia ya watu waandamana Berlin Ujerumani kuunga mkono haki za Wapalestina
Mamia ya watu mjini Berlin, Ujerumani wameandamana kwa ajili ya kuunga mkono haki za Wapalestina, ambao wamekuwa wakilengwa na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala haramu wa Israel.
Maandamano hayo ambaye yamefanyika kwa mnasaba wa mwaka wa tatu tangu kuanza vita vya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, yameshuhudia waandamanaji wakipiga nara dhidi ya Israel na Marekani na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhlumu wa Palestina.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za Palestina, wametoa wito wa kukomeshwa vita vya Gaza, utawala wa Israel uwajibishwe kwa uhalifu wa kivita, na Ujerumani iache kuupatia silaha utawala ghasibu wa Israel unaoendelea kufanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao walisisitiza haki ya Wapalestina ya kupinga ukaliaji wa mabavu wa ardhi zao unaofanywa na utawala wa Israel, wakisema: “Kusalimu amri kamwe si chaguo.”
Hayo yanajiri klatika hali ambayo, maadhimisho ya miaka mitatu ya operesheni ya "Kimbunga cha al-Aqswa" yalifanyika Jumatano Oktoba 7 huku ikionekana wazi kwamba eneo la Asia Magharibi litaendelea kuishi katika mazingira yaliyotawaliwa na athari endelevu za tukio hilo la kihistoria la Kumbunga cha al Aqsa.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, jeshi katili la Isarel limefanya unyama, ukatili na jinai za kuchupa mipaka. Limeua makumi ya maelfu ya raia, limefanya uharibifu wa mfumo mzima wa maisha huko Gaza, limetanua vita hadi maeneo mengine na kuanzisha kampeni kubwa na pana ya ukatili katika eneo hili zima, lakini kila leo jinamizi la Oktoba 7 linazidi kuwa kubwa na zito kwa utawala wa Kizayuni.
Baadhi ya wachambuzi na duru za uchanganuzi wa matukio wanasema kuwa, mashambulizi makubwa na ya kikatili yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni yameshindwa kufuta aibu na fedheha ya kihistoria uliyopata kutokana na operesheni ya Kimbunga cha al Aqswa na umeshindwa kujionesha mbele ya walimwengu kuwa una nguvu zisizoshindika.