Sep 05, 2016 07:34 UTC
  • Ayatullah Shirazi: Uwahabi ni tishio kubwa zaidi kwa Uislamu na Ubinadamu

Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Iran amesema hii leo Uwahabi una wafuasi wanaotenda jinai na wasio na huruma hata kidogo na hivyo ni hatari kubwa zaidi kwa Uislamu na ubinadamu.

Ayatullah Nasser Makarim Shirazi Marjaa Taqlid aliye katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran aliyasema hayo Jumapili katika hafla ya kuanza mwaka mpya wa masomo shuleni na vyuo vya kidini. Ameongeza kuwa, katika hali ya hivi sasa, makundi ya Mawahabi wakufurishaji yanaaibisha Uislamu kote duniani kwa uharibifu na jinai wanazotenda. Amesema kuna haja ya kuwafahamisha Waislamu na walimwengu kwa ujumla kuwa Mawahabi hawafuati Uislamu.

Ameongeza kuwa, ni lazima kufichua ukweli kuhusu Uwahabi ili vijana wasitumbukie katika mtego wa Uwahabi na makundi ya kigaidi kama vile Daesh au ISIS. Ayatullah Makarim Shirazi amesema, Maulamaa wa Kisuni na Kishia tayari wameshaazisha harakati za kutoa maelezo kuhusu Uwahabi. Amesema hivi karibuni Maulamaa wa Kisunni  duniani walishiriki katika kongamano katika Jamhuri ya Chechnia na kutangaza kuwa Mawahabi si Waislamu jambo ambalo liliwakasirisha sana watawala wa Saudia na wasomi wa Kiwahabi.

Magaidi wa ISIS

Mwanazuoni huyo wa ngazi za juu nchini Iran amesema Waislamu wanapaswa kuwafahamisha walimwengu kuwa Uislamu si dini ya vita. Amesema hivi haribuni alimshukuru Papa Francis baada ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kusema ISIS haina uhusiano na Uislamu na Waislamu.

Ayatullah Makarim Shirazi ameelezea matumaini yake kuwa, Uwahabi utaangamia na kwa njia hiyo matatizo yote ya Waislamu, yakiwmo kuhusu Hija, yatatatuliwa.

Tags