Saudia na Israel zashirikiana katika marasimu ya Hija ya mwaka huu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15127-saudia_na_israel_zashirikiana_katika_marasimu_ya_hija_ya_mwaka_huu
Utawala wa Kizayuni wa Israel unashirikiana na Saudi Arabia katika marasimu ya ibada ya Hija mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 11, 2016 09:57 UTC
  • Saudia na Israel zashirikiana katika marasimu ya Hija ya mwaka huu

Utawala wa Kizayuni wa Israel unashirikiana na Saudi Arabia katika marasimu ya ibada ya Hija mwaka huu.

Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa, Saudi Arabia imezidisha hatua zake za kiusalama katika marasimu ya Hija ya mwaka huu  katika kile kilichotajwa na utawala huo kuwa imefanya hivyo kwa lengo la kuzuia kukaririwa maafa ya Mina. Imeelezwa kuwa mahujaji katika ibada ya Hija mwaka huu huko Saudia wanapasa kuvaa mikononi vifaa vya elektroniki vilivyotengenezwa na kampuni moja ya Israel, vifaa ambavyo vina taarifa za mtu binafsi na za kitiba za kila hujaji.

Mahujaji wakiwa katika jangwa la Arafa

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kamera mia nane zimewekwa pia katika maeneo matakatifu huko Saudi Arabia. Redio moja ya Israel hivi karibuni iliripoti kuwa, kufuatia kusainiwa makubaliano kati ya Saudia na kampuni hiyo ya Israel, mahujaji watakuwa wakidhibitiwa mienendo na miamala yao na vifaa hivyo vya kielektroniki vinavyofungwa mikononi tokea wanapowasili kwenye viwanja vya ndege huko Saudia hadi wanaporejea makwao.

Ibada ya Hija ya mwaka huu inafanyika bila ya kudhuhuriwa na mahujaji kutoka Iran, Yemenn na Syria. Utwala wa Aal Saud umewazuia mahujaji wa baadhi ya nchi za Kiislamu ikiwemo Iran kushiriki katika Hija ya Ibrahim ya mwaka huu kwa sababu zisizo na msingi wowote. Maelfu ya Mahujaji wakiwemo 464 wa Iran waliaga dunia mwaka jana wakati walipokuwa katika amali za Hija huko Mina kutokana na usimamizi mbovu wa maafisa wa Aal Saud.