Mahmoud Abbas akariri madai ya kujiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16240-mahmoud_abbas_akariri_madai_ya_kujiuzulu
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa mara nyingine amekariri madai yake ya kujiuzulu wadhifa huo.
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Sep 28, 2016 04:22 UTC
  •  Mahmoud Abbas  akariri madai ya kujiuzulu

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa mara nyingine amekariri madai yake ya kujiuzulu wadhifa huo.

Mahmoud Abbas jana aliwaandikia barua ya malalamiko wakuu wa baadhi ya nchi za Kiarabu na kudai kuwa, atajiuzulu nafasi ya Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, iwapo viongozi wa Kiarabu wataendelea kuingilia masuala ya ndani ya Palestina na ya makundi ya Kipalestina khususan kuingilia masuala ya harakati ya Fat-h ambayo anaiongoza. Hii ni katika hali ambayo matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimaidani cha Palestina yanaonyesha kuwa, theluthi mbili ya Wapalestina wanamtaka Mahmoud Abbas ajiuzulu.

Mahmoud Abbas (kushoto) akiwa na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni 

Wapalestina wengi wanaitambua Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuwa ni mzigo tu kwa wananchi hao huku wakimtuhumu Abbas kuwa anashirikiana na utawala wa Kizayuni unaotenda jinai dhidi ya raia hao; na kwa msingi huo wanataka ajiuzulu.