Raia wa Syria watumiwa kama ngao ya binadamu
Raia zaidi ya 100 wameuawa huko Syria katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Watetezi wa Haki za Binadamu huko Syria Jumatatu wiki hii wametoa ripoti na kukiri kuwa magaidi waliwatumia raia wa Syria kama ngao ya binadamu katika maeneo palipokuwa pakijiri mapigano na kwamba Wasyria zaidi ya elfu moja wameuawa katika mapigano mwezi uliopita wa Septemba nchini humo.
Ripoti hiyo ya Watetezi wa Haki za Binadamu imeongeza kuwa, Wasyria 1180 wameuawa vitani mwezi Septemba mwaka huu; huku asilimia karibu sitini ya waliouliwa wakiwa ni wanawake na watoto.
Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu pia kimekiri pia kuwa, takwimu sahihi za raia waliouliwa huko Syria wakitumiwa na magaidi kama ngao ya binadamu ni zaidi ya hii iliyotolewa. Baadhi ya maeneo ya Syria yamekumbwa na hali ya mchafukoge kufuatia kuwepo makundi ya kigaidi tangu miaka mitano iliyopita hadi sasa.