Houthi: Saudia wanashirikiana na al-Qaeda Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1774-houthi_saudia_wanashirikiana_na_al_qaeda_yemen
Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Saudi Arabia na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda zinashirikiana katika mashambulizi yao ya kutisha nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2016 04:26 UTC
  • Houthi: Saudia wanashirikiana na al-Qaeda Yemen

Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Saudi Arabia na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda zinashirikiana katika mashambulizi yao ya kutisha nchini Yemen.

Akizungumza jana Jumatatu kutoka mkoa wa Sa'ada, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu, al-Houthi amesema wana ushahidi unaoonyesha kuwa Saudia, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinashirikiana na magaidi wa al-Qaeda katika kendeleza hujuma zao za kikatili nchini humo.

Hii ni katika hali ambayo, ripoti iliyochapishwa na shirika la habari la BBC imebainisha kwamba vikosi vya Saudia vinafanya kazi bega kwa bega na magaidi wa kundi Ansar al-Sharia, ambalo ni tawi la mtandao wa al-Qaeda katika Peninsula ya Kiarabu, kusini magharibi mwa Yemen na hususan katika mkoa wa Ta'izz. Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen tarehe 26 mwezi Machi mwaka jana 2015, lengo likiwa ni kuisambaratisha harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Rais mtoro wa Yemen Abdu-Rabuh Mansour Hadi.