Magaidi 500 wauawa, 1000 wajeruhiwa Aleppo chini ya masaa 24
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18433-magaidi_500_wauawa_1000_wajeruhiwa_aleppo_chini_ya_masaa_24
Mamia ya magaidi wameangamizwa na jeshi la Syria likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi mjini Aleppo, kusini mashariki mwa nchi, chini ya masaa 24 yaliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 30, 2016 03:43 UTC
  • Magaidi 500 wauawa, 1000 wajeruhiwa Aleppo chini ya masaa 24

Mamia ya magaidi wameangamizwa na jeshi la Syria likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi mjini Aleppo, kusini mashariki mwa nchi, chini ya masaa 24 yaliyopita.

Kanali ya televisheni ya al-Mayadeen imesema magaidi 500 wameuawa na wengine 1000 kujeruhiwa vibaya katika makabaliano makali ya kuukomboa mji huo yaliyoanza Ijumaa. Hata hivyo jeshi la Syria halijatoa taarifa na takwimu rasmi kuhusu makabiliano hayo.

Usiku wa kuamkia leo, jeshi la Syria limefanikiwa kuzima mashambulizi ya magenge ya kigaidi katika wilaya ya Al-Zahraa.

Vikosi vya Syria mjini Aleppo

Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi vya jeshi la anga la Russia hivi karibuni lilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya kuwatimua magaidi katika mji wa Aleppo ambapo hadi sasa maelfu ya magaidi wa Daesh na wa makundi mengine ya kigaidi wameuliwa na wengine karibu 2500 kujeruhiwa.

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya milioni moja na laki saba wamefanikiwa kuyakimbia maeneo ambayo ni ngome za magenge hayo ya kigaidi na kukimbilia maeneo salama ambayo yako chini ya serikali, magharibi mwa nchi.