Jibu la Iraq dhidi ya madai yasiyo na msingi ya Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i20158-jibu_la_iraq_dhidi_ya_madai_yasiyo_na_msingi_ya_saudia
Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq ilitoa jibu dhidi ya matamshi ya Thamer Al-Sabhan, Waziri Mshauri wa Saudia katika masuala ya nchi za Ghuba ya Uajemi, ikisema kuwa wizara hiyo ya kigeni ya Iraq ni mali ya Wairaq wote.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 25, 2016 08:21 UTC
  • Jibu la Iraq dhidi ya madai yasiyo na msingi ya Saudia

Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq ilitoa jibu dhidi ya matamshi ya Thamer Al-Sabhan, Waziri Mshauri wa Saudia katika masuala ya nchi za Ghuba ya Uajemi, ikisema kuwa wizara hiyo ya kigeni ya Iraq ni mali ya Wairaq wote.

Ahmad Jamal, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq alisema kuwa, kutumia vibaya jina la Makka Takatifu kwa ajli ya kufikia malengo ya kisiasa kunakofanywa na Saudia ni shara ya kushindwa na kufeli utendaji wa Al-Sabhan. Amesisitiza kuwa, baada ya kuondolewa Thamer Al-Sabhan nchini Iraq bado afisa huyo wa Saudia hajaelewa kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya taifa ni mali ya Wairaq wote na si vinginevyo.

Inafaa kukumbusha kuwa, Al-Sabhan ambaye alikuwa nchini Iraq kama balozi wa Saudia na kutimuliwa na serikali ya Baghdad kutokana na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, ametoa tuhuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje ya Iraq, Ibrahim al-Jaafari kwamba tangu awali alikuwa na fikra za kuiharibu Makka. Matamshi ya uingiliaji wa Thamer Al-Sabhan yanarudi nyuma hadi kwenye kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu OIC. Katika kikao hicho ambacho kilipewa anwani ya kulaani kile ambacho Saudia ilikitaja kuwa ni shambulizi la kombora la harakati ya Answarullah ya Yemen dhidi ya Makka, sanjari na kutolewa azimio la kulaani suala hilo, Baghdad kupitia waziri wake wa mashauri ya kigeni alipiga kura ya kupinga madai hayo ya Saudia.

Thamer Al-Sabhan, aliyekuwa balozi wa Saudia nchini Iraq na kutimuliwa

Kadhalika Ibrahim al-Jaafari alilaani hatua ya Riyadh ya kutoa tuhuma dhidi ya harakati hiyo bila ya kuwa na uthibitisho wowote.

Shambulizi la jeshi la Yemen lililoulenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jeddah katika kulipiza kisasi uvamizi wa Riyadh dhidi ya nchi hiyo, liliwatia kiwewe watawala wa Aal-Saud ambao walianzisha propaganda chafu zenye lengo la kuchochea hisia za Waislamu duniani. Viongozi wa Saudia ambao wanashikilia uongozi wa maeneo matatifu ya Kiislamu, huku wakiwa wameonyesha kutokuwa na uwezo wa kusimamia maeneo hayo, hivi sasa wanajaribu kuzipotosha fikra za walio wengi juu ya kadhia hiyo. Kwa kueneza propaganda ya kile wanachokitaja kuwa ni wahudumu wa maeneo matakatifu nchini Saudia, Aal-Saud wameweza kulinda maslahi yao ya kisiasa ndani na nje ya nchi hiyo.

Ibrahim al-Jaafari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq

Aidha kutolewa tuhuma hizo zisizo na msingi wowote dhidi ya harakati hiyo ya Answarullah, Saudia inakusudia kuendeleza vita na uingiliaji wake katika eneo la Mashariki ya Kati.

Hakuna shaka kwamba, kwa kutumia propaganda za uhudumu wa al-Kaabah na Masjidul-Haram mjini Makka na kadhalika Msikiti wa Mtume (saw) mjini Madina, viongozi hao wa Saudia wameweza kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi. Kwa kuzingatia kuwa, Makka na Madina ni maeneo yenye kuheshimiwa sana na Waislamu, watawala wa kifalme wa Saudia wanayatumia maeneo hayo matukufu kwa ajili ya kufikia malengo yao machafu.

Kombora la Burkan la jeshi la Yemen lililowatia tumbo joto watawala wa Saudia

Katika fremu hiyo miongo kadhaa ya hivi karibuni na kwa kutumia masuala kama nafasi yake ya kijografia, pato kubwa litokanalo na mafuta na kadhakika kuwepo miji ya Makka na Madina ndani ya ardhi ya nchi hiyo, Riyadh imekuwa ikijaribu kutwaa uongozi wa ulimwengu wa Kiislamu na kuwatwisha mitazamo yake ulimwengu huo. Wasaud wenye kufuata fikra za Kisalafi na Kiwahabi kama idolojia yao maalumu ya kisiasa, wanajitahidi kuwa na satwa na ushawishi katika eneo zima la Mashariki ya Kati sanjari na kueneza itikadi hizo kwa wWaisalmu wa eneo hilo na maeneo mengine ya dunia.

Uwanja wa ndege wa Abdulaziz mjini Jeddah Saudia, ulioshambuliwa kwa kombora la Burkan

Fikra hizo si tu kwamba zinahatarisha eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla kutokana na kuzalisha makundi ya ukufurishaji na kigaidi, bali ni kwamba zinapingana kikamilifu na Uislamu halisi. Ni kwa kupitia fikra hizo ndio kukapelekea kuharibiwa maeneo matakatifu nchini Syria na Iraq kupitia fremu ya njama za kuharibu alama za Kiislamu, njama zinazoratibiwa nchini Saudia. Ndio maana viongozi wa Iraq kwa kufahamu ukweli huo, wakatoa radiamali kali kwa hatua ya viongozi wa Saudia ya kutumia vibaya maeneo matakatifu kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kisiasa.