Juhudi zilizofeli za Saudi Arabia huko Yemen
Juhudi za jeshi la Saudi Arabia za kuukomboa mji wa al Rabia katika mkoa wa Asir kusini mwa nchi hiyo zimegonga mwamba hadi sasa.
leo Jumatano jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen vimekabiliana pakubwa na kuzuia shambulio la vikosi vya Saudia kwa ajili ya kuuukomboa mji wa al Rabia katika mkoa wa Asir. Katika oparesheni hiyo vikosi vya Saudi Arabia vimepata hasara na maafa makubwa. Wanajeshi kadhaa wa Saudia wameuliwa kwenye shambulio hilo.
Vikosi vamizi vya Saudi Arabia pia vimeyashambulia kwa makombora na mizinga maeneo kadhaa ya mkoa wa mpakani wa Jizan na kuyashambulia pia maeneo ya al Makhruq na al Sharqiya katika mkoa wa mpakani wa Najran.
Televisheni ya al Aalam imeripoti kuwa jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen vimevurumisha makombora katika kambi ya kijeshi ambako vilikuwepo vikosi vamizi vya Saudia na vibaraka wao katika mkoa wa Maarib katikati mwa Yemen. Katika shambulio hilo mamluki kadhaa wa Saudia wameuawa na kujeruhiwa.