UN: Wayemen milioni 19 wanahitaji misaada ya dharura
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i23557-un_wayemen_milioni_19_wanahitaji_misaada_ya_dharura
Umoja wa Mataifa umesema takriban watu milioni 19 wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu nchini Yemen.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 16, 2017 00:21 UTC
  • UN: Wayemen milioni 19 wanahitaji misaada ya dharura

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu milioni 19 wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu nchini Yemen.

Shirika la habari la Russia Today limeripoti kuwa, mamilioni ya Wayemen wanapitia kipindi kigumu cha kukosa mahitaji muhimu ya msingi kama vile chakula na matibabu na hususan katika wilaya ya Tuhayat, katika pwani ya bahari Nyekundu. 

Takwimu za UN zimebainisha kuwa, zaidi ya watoto milioni 1.5 katika eneo hilo wapo katika ncha ya kupoteza maisha kutokana na njaa na utapiamlo.

Watoto wa Yemen wakitafuta mabaki ya chakula jalalani

Umoja wa Mataifa umesema watoto zaidi ya milioni 12 wanakodolewa macho na njaa katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu.

Hii ni katika hali ambayo, mapema mwezi huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliripoti kuwa hali ya kiafya nchini Yemen ni mbaya sana na kubainisha kuwa tangu vilipoanza vita vya Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo hadi mwezi Novemba mwaka jana, zaidi ya watu 7,300 wameuawa na wengine 39,000 kujeruhiwa, mbali na vituo 274 vya afya ambavyo vimeharibiwa au kubomolewa kikamilifu.

Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka 2015, kwa uungaji mkono wa Marekani, Saudi Arabia ilianzisha mashambulio dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen. Moja kati ya malengo makuu ya mashambulio hayo ya kivamizi ya utawala wa Aal Saud ni kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake, rais aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abdurabbuh Mansur Hadi. 

Hali ya ukame nchini Yemen