Watoto elfu mbili wahanga wa uvamizi wa kijeshi wa Saudia Yemen
Mratibu wa Oparesheni za Masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa watoto wasiopungua elfu mbili wameuawa na kujeruhiwa huko Yemen tangu Saudi Arabia ianzishe mashambulizi ya kijeshi nchini humo mwaka uliopita.
Stephen O' Brien amesisitiza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba watoto wasiopungua 90 wameuawa katika mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake huko Yemen tangu kuanza mwaka huu wa 2016 pekee.
O'Brien ameongeza kuwa, Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) na taasisi nyingine kwa miezi kadhaa sasa zinafanya juhudi kufikisha misaada ya kibinadamu huko Yemen.
Stephen O'Brien pia ametahadharisha kuhusu hatua yoyoye iitakayozorotesha mchakato wa ufikishaji misaada ya kibinadamu kupitia bandari za Yemen.
Mtaribu wa Oparesheni za Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa mwezi uliopita aliwahi kusema kuwa muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia unazuia kufikishwa misaada kwa wananchi wa Yemen ambao asilimia 80 kati yao wanahitaji misaada ya kibinadamu.