Mamia ya Wazayuni wakivamia tena Kibla cha Kwanza cha Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24657-mamia_ya_wazayuni_wakivamia_tena_kibla_cha_kwanza_cha_waislamu
Vyombo vya habari vya Palestina vimetangaza habari isemayo kuwa, zaidi ya walowezi 370 wa Kizayuni wameuvamia Msikiti wa al Aqsa, ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, wiki iliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2017 00:25 UTC
  • Mamia ya Wazayuni wakivamia tena Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Vyombo vya habari vya Palestina vimetangaza habari isemayo kuwa, zaidi ya walowezi 370 wa Kizayuni wameuvamia Msikiti wa al Aqsa, ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, wiki iliyopita.

Shirika la habari la Quds la Palestina limetangaza kuwa, kuanzia tarehe 29 mwezi ulioisha wa Januari hadi juzi tarehe pili Februari, walowezi 373 wameuvamiza Msikiti wa al Aqsa kwa uungaji mkono kamili wa polisi na shirika la kijasusi na usalama wa ndani la Israel, na kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.

Katika uvamizi wao wote ambao wamekuwa wakiufanya kila siku isipokuwa Ijumaa na Jumatamosi, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakiingia msikitini humo kwa kutumia mlango wa "Bab al Maghariba" na kutokea mlango wa "Bab al Silsilah."

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo hivyo vya habari vya Palestina, mwezi Januri mwaka huu, walowezi 1715 wa Kizayuni walikivamia Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu.

Walowezi wa Kizayuni wakiendelea kuvunjia heshima matukufu ya kidini kwa msaada wa jeshi la polisi na maafisa usalama wa Israel.

 

Eneo hilo takatifu limegeuzwa na Wazayuni kuwa mahali pa kuoneshea ujuba wao kwa lengo la kuangamiza utambulisho wa Kiislamu wa eneo hilo.

Jinai hizo za Wazayuni haziishii tu kuharibu matukufu ya Waislamu, bali Israel inaharibu pia matukufu ya Wakristo wa Palestina na inafanya njama za kila namna kufuta athari zote za Kiislamu na Kikristo za mji mtakatifu wa Quds.

Ikumbukwe kuwa, uchokozi wa hivi karibuni wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa, umepelekea kuanza Intifadha ya Tatu ya Wapalestina.