Israel inataka kujenga kisiwa katika pwani ya Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26366-israel_inataka_kujenga_kisiwa_katika_pwani_ya_ghaza
Kanali ya kwanza ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa waziri wa usafirishaji wa Israel amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa nchi za Kiarabu kwa minajili ya kuchunguza mpango wa kujenga kisiwa karibu na pwani ya Ukanda wa Ghaza katika kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti zaidi Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2017 03:47 UTC
  • Israel inataka kujenga kisiwa katika pwani ya Ghaza

Kanali ya kwanza ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa waziri wa usafirishaji wa Israel amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa nchi za Kiarabu kwa minajili ya kuchunguza mpango wa kujenga kisiwa karibu na pwani ya Ukanda wa Ghaza katika kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti zaidi Wapalestina.

Kanali ya habari ya al Aalam yenye makao yake hapa Tehran imemnukuu ripota wa kanali ya kwanza ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ambaye ameeleza kuwepo mpango wa kujenga kisiwa karibu na pwani ya Ukanda wa Ghaza na kuongeza kwamba, Yisrael Katz, waziri wa usafirishaji wa utawala wa Kizayuni tangu miezi kadhaa iliyopita amekuwa akitafuta ufadhili wa fedha ili kutekeleza mpango wa ujenzi wa kisiwa hicho katika pwani ya Ukanda wa Ghaza katika umbali wa kilomita 4.5 kutoka katika fukwe za ukanda huo na chenye ukubwa wa kilomita mraba 7 hadi 8. Gazeti la Kizayuni la Haaretz pia limeandika kuwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni naye anaunga mkono kujengwa kisiwa hicho katika pwani ya Ukanda wa Ghaza. 

Sehemu ya Eneo la Pwani ya Ghaza inayoonekana kutokea juu

Katz kwa mara ya kwanza alitoa pendekezo hilo la kujenga kisiwa hicho mwaka 2014 na sasa anatafuta uungaji mkono wa kifedha ili kufanikisha ujenzi huo. Waziri huyo wa usafirishaji wa Israel amesema kuwa, tayari amepata wafadhili wa kifedha kutoka Saudi Arabia na China ambacho inaonekana wazi kuwa lengo lake ni kuwadhibiti Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.