Wazayuni wawateka nyara Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameyavamia maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwateka nyara Wapalestina kadhaa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni leo wamewateka nyara Wapalestina kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana.
Jana Ijumaa pia, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walivamia maandamano ya Wapalestina katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi na kujeruhi Wapaelstina wasiopungua 60.
Wapalestina hao walikuwa wameitisha maandamano hayo ili kuwaunga mkono Wapalestina wenzao waliogoma kula katika jela za kutisha za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mara kwa mara Wazayuni wamekuwa wakiwakandamiza kwa njia tofauti Wapalestina na kufanya ukatili mkubwa dhidi yao kwa shabaha ya kuwanyamazisha na kufanikisha malengo yao haramu.
Wapalestina zaidi ya 300 wameshauawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni yaliyoanza mwezi Oktoba 2015, yaani baada ya kuanza Itifadha ya Quds hadi hivi sasa.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea pia kupora ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye maeneo hayo, licha ya dunia nzima kulalamikia jinai hizo.