Wazayuni waendelea kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i30470-wazayuni_waendelea_kukivunjia_heshima_kibla_cha_kwanza_cha_waislamu
Makumi ya walowezi wa Kizayuni jana Jumatano waliuvamia tena msikiti wa al Aqswa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 14, 2017 21:59 UTC
  • Wazayuni waendelea kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Makumi ya walowezi wa Kizayuni jana Jumatano waliuvamia tena msikiti wa al Aqswa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Palestina, walowezi hao wa Kizayuni wameuvamia msikiti wa Aqsa kwa kupitia lango la "Bab al Maghariba" wakiwa wamepewa ulinzi mkubwa na wanajeshi na maafisa usalama wa Israel.

Masjidul Aqswa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Mapema jana asubuhi, askari wa utawala vamizi wa Israel walitumwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuwafungulia njia walowezi wa Kizayuni kuuvamia msikiti wa Aqsa.

Lengo la utawala wa Kizayuni ni kuwapokonya Waislamu Kibla chao cha kwanza na wanafanya njama za kila namna za kuuyahudisha mji wa Baytul Muqaddas na kuwazuia Waislamu kufanya ibada kwenye msikiti huo.

Walowezi wa Kizayuni wakivamia maeneo matakatifu ya Waislamu kwa msaada wa maafisa usalama wa Israel

 

Pamoja na hayo lakini, mamia ya Waislamu wa Palestina kutoka maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanamiminika kwenye eneo hilo hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kufanya ibada.

Itakumbukwa pia kuwa, Intifadha ya Tatu ya Wapalestina iliyoanza tarehe Mosi Oktoba 2015, ilianza baada ya wanajeshi na walowezi wa Kizayuni kuzidisha jeuri zao dhidi ya matukufu ya Kiislamu huko Palestina. Intifadha hiyo imepewa jina la Intifadha ya Masjidul Aqswa. Hadi hivi sasa zaidi ya Wapalestina 315 wameshauliwa shahidi na askari makatili wa Israel tangu ilipoanza Intifadha hiyo.