Wazayuni wandelea kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33736-wazayuni_wandelea_kukivunjia_heshima_kibla_cha_kwanza_cha_waislamu
Walowezi wa Kizayuni wameuvamia kwa mara nyingine tena Msikiti wa al Aqsa na kukivunjia heshima Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 28, 2017 10:52 UTC
  • Wazayuni wandelea kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Walowezi wa Kizayuni wameuvamia kwa mara nyingine tena Msikiti wa al Aqsa na kukivunjia heshima Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu.

Kituo cha habari cha Palestina kimetangaza habari hiyo mjini Quds na kuongeza kuwa, walowezi wa Kizayuni leo wameingia msikitini humo na kukagua sehemu zake mbalimbali huku wakipiga picha ili wachochee hasira za Waislamu.

Walowezi hao wa Kizayuni wameingia katika Msikiti wa al Aqsa kwa kupitia lango la al Maghariba, wakiwa na ulinzi mkali wa wanajeshi wa Israel.

Wakati huo huo Waislamu wa Palestina pamoja na wanafunzi wa kidini waliokuwemo msikitini humo wameshindwa kuvumilia jeuri hiyo ya Wazayuni na wamesimama imara kukabiliana nao na kuwalazimisha kutoka msikitini humo.

 

Ripoti ya taasisi ya kimataifa ya Quds inaoensha kuwa karibu walowezi 23 elfu na 661 wa Kizayuni wameuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa tangu mwezi Agosti mwaka 2016 hadi Agosti mwaka huu. Kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 58 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.

Wazayuni hawaheshimu kabisa maeneo matakatifu ya Waislamu bali hata ya Wakristo huko Palestina na mara kwa mara wanavunjia heshima matukufu ya kidini kwa uungaji mkono kamili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jeuri hizo za Wazayuni zilipelekea kuanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba 2015 na zaidi  ya Wapalestina 350 wameshauawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa tangu ilipoanza Intifadha hiyo.