Vibara 80 wa Saudia wauawa nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3484-vibara_80_wa_saudia_wauawa_nchini_yemen
Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limetoa pigo kubwa na kuwashinda vibaraka wa Saudi Arabia katika eneo la Taiz na kuua 80 miongoni mwao licha ya kusaidiwa na ndege za kivita za utawala wa kifalme wa Aal Saud na washirika wao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 20, 2016 23:04 UTC
  • Vibara 80 wa Saudia wauawa nchini Yemen

Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limetoa pigo kubwa na kuwashinda vibaraka wa Saudi Arabia katika eneo la Taiz na kuua 80 miongoni mwao licha ya kusaidiwa na ndege za kivita za utawala wa kifalme wa Aal Saud na washirika wao.

Taarifa iliyotolea jana na jeshi la Yemen imesema kuwa jeshi hilo la makundi ya kujitolea ya wananchi yamefanikiwa kuua vibaraka 80 wa Saudia katika operesheni ya aina yake kwenye eneo la al Dhabab. Imesema Kanali Muhammad Abdullah al Auni ambaye ni kati ya makamanda wa kikosi cha 35 cha vibara wa Saudia ni miongoni mwa waliouangamizwa katika operesheni hiyo. Vilevile Yahya Mabhit na Abu Ubaida al Haddi ambao ni miongoni mwa viongozi wa kundi la al Qaida wameuawa katika operesheni hiyo ya aina yake na makumi ya vibaraka wengine wamejeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Yemen, Saba, imesema kuwa baadhi ya waliouawa katika operesheni hiyo walikuwa wakisakwa na Kamati ya Wananchi wa Yemen.

Saudi Arabia na washirika wake walianza mashambulizi makali ya anga na nchi kavu dhidi ya taifa la Yemen Machi mwaka jana kwa shabaha eti ya kumrejesha madarakani rais aliyetoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi. Maelfu ya Waislamu wa Yemen wameuawa hadi sasa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi.