Israel yakiri shirika lake la kijasusi linafanya uharibifu Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34917-israel_yakiri_shirika_lake_la_kijasusi_linafanya_uharibifu_afrika
Kwa mara ya kwanza utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwa, umekuwa ukifanya uharibifu barani Afrika kama vile vitendo vya kigaidi kwa shabaha ya kuwatisha na kuwachochea Mayahudi.
(last modified 2026-05-13T18:57:29+00:00 )
Sep 27, 2017 06:29 UTC
  • Israel yakiri shirika lake la kijasusi linafanya uharibifu Afrika

Kwa mara ya kwanza utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwa, umekuwa ukifanya uharibifu barani Afrika kama vile vitendo vya kigaidi kwa shabaha ya kuwatisha na kuwachochea Mayahudi.

Shirika la habari la FARS limeripoti kuwa, katika hatua ambayo haijawahi kutokea, kanali ya pili ya televisheni ya Israel mwishoni mwa wiki na baada ya kupita miaka 64 ilifichua jinai zilizofanywa na magaidi wa shirika la kijasusi la Israel MOSSAD katika nchi za kaskazini mwa Afrika. Kwa mujibu wa televisheni hiyo, shirika la kijasusi la Israel liliunda vijikundi vya siri vya kijeshi na kijasusi katika eneo lote la kaskazini mwa Afrika ili kuwatia hofu Mayahudi na kuwachochea wahamie katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Shirika la kijasusi la Marekani MOSSAD

 

Wakati huo huo, kituo cha takwimu cha utawala wa Kizayuni kwa mara ya kwanza kimetoa takwimu za mwaka 2009 hadi 2015 na kusema kuwa, idadi ya Wazayuni wanaozikimbia ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu imepindukia ile ya wanaohamia katika ardhi hizo.

Kwa mujibu wa kituo hicho, kila mwaka idadi ya Wazayuni wanaokimbia ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu inaongezeka. Sababu mbalimbali zikiwemo za ugumu wa maisha, ufisadi wa kimaadili, ubadhirifu wa fedha na ukosefu mkubwa wa amani na usalama ni sababu kubwa inayowafanya Wazayuni hao kuzikimbia ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.