Jeshi la Iraq laukomboa mji wa Hawija kutoka makucha ya ISIS
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i35251-jeshi_la_iraq_laukomboa_mji_wa_hawija_kutoka_makucha_ya_isis
Jeshi la Iraq limetangaza kuukomboa mji wa kistratijia wa Hawija kutoka katika makucha ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 05, 2017 04:34 UTC
  • Jeshi la Iraq laukomboa mji wa Hawija kutoka makucha ya ISIS

Jeshi la Iraq limetangaza kuukomboa mji wa kistratijia wa Hawija kutoka katika makucha ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo Alhamisi, Jeshi la Iraq limesema mji wa Hawija ulio katika mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Kirkuk kaskazini mwa nchi hiyo, umekombolewa baada ya wiki kadhaa za mapigano makali na magaidi wa ISIS waliokuwa wameteka mji huo.

Taarifa zinasema kufuatia kukombolewa Hawija, hivi sasa eneo pekee ambalo limebakia mikononi mwa ISIS ni kipande kidogo cha mpaka wa magharibi mwa Iraq na Syria. Awamu ya kwanza ya kuukomboa mji wa Hawija, ulio umbali wa kilomita 300 kutoka Baghdad, ilianza Septemba 21. Mnamo Septemba 29 Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi alitangaza kuanza awamu ya pili ya oparesheni ya kuukomboa mji huo.