Syria: Kamwe hatutaruhusu kushambuliwa Hizbullah ya Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36252-syria_kamwe_hatutaruhusu_kushambuliwa_hizbullah_ya_lebanon
Mshauri wa Rais wa Syria amesisitiza kuwa, mahusiano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hizbullah na Syria ni ya kiwango cha juu na kusema Damascus kamwe haitaruhusu harakati hiyo ya Kiislamu ya Hizbullah ishambuliwe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2017 11:43 UTC
  • Syria: Kamwe hatutaruhusu kushambuliwa Hizbullah ya Lebanon

Mshauri wa Rais wa Syria amesisitiza kuwa, mahusiano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hizbullah na Syria ni ya kiwango cha juu na kusema Damascus kamwe haitaruhusu harakati hiyo ya Kiislamu ya Hizbullah ishambuliwe.

Bouthaina Shaaban amesema kuwa, Syria haiwezi kuruhusu kitu hicho kwa kuwa mustakbali wa Syria unafungama sana na harakati ya Hizbullah. Shaaban aliyeyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Mayadin ya nchini Lebanon amefafanua kuwa, Syria haitosita hata kidogo katika kujilinda mbele ya sera za kupenda kujitanua za utawala khabithi wa Israel.

Wanamuqawama wa Hizbullah

Kadhalika mshauri wa Rais wa Syria ameweka wazi njama za utawala haramu wa Israel za kuzusha migogoro nchini kwake na kusema kuwa, Israel imethibitisha kwamba ina historia ya muda mrefu ya kuanzisha vita dhidi ya Syria na hivi sasa inajitahidi kutumia vibaya vita vya ndani vilivyoibuliwa na baadhi ya nchi za ndani na nje ya eneo la Mashariki ya Kati. 

Njama chafu za US na Israek dhidi ya Syria

Bouthaina Shaaban pia amezungumzia kitendo cha kujiuzulu waziri mkuu wa Lebanon, Saad Hariri akiwa nchini Saudia na kusema kuwa, hatua ya Hariri ya kujiengua kutoka serikali ya Lebanon tena akiwa ndani ya nchi nyingine hairidhishi.