Nchi 70 kushiriki katika mkutano wa kuijenga upya Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39921-nchi_70_kushiriki_katika_mkutano_wa_kuijenga_upya_iraq
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imetangaza kuwa, nchi 70 na mamia ya mashirika makubwa na wewekezaji wa kimataifa wametangaza nia yao ya kushiriki katika mkutano wa kuijenga upya Iraq unaotarajiwa kufanyika Kuwait baadaye mwezi huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 05, 2018 01:08 UTC
  • Nchi 70 kushiriki katika mkutano wa kuijenga upya Iraq

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imetangaza kuwa, nchi 70 na mamia ya mashirika makubwa na wewekezaji wa kimataifa wametangaza nia yao ya kushiriki katika mkutano wa kuijenga upya Iraq unaotarajiwa kufanyika Kuwait baadaye mwezi huu.

Ahmad Mahjoub, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, inatabiriwa kwamba katika mkutano huo, serikali ya Iraq itaweza kukusanya msaada wa karibu dola bilioni 100 pamoja na uwekezaji wa kimataifa wa kuyajenga upya maeneo mbalimbali ya nchi hiyo yaliyoharibiwa vibaya na vita.

Miji ya Iraq imeharibiwa vibawa kwa vita vya ndani

 

Amesema, asasi za kijamii, mashirika mbalimbali na nchi tofauti zitakazoshiriki kwenye mkutano huo, zitajadiliana njia na namna ya kuwekeza nchini Iraq.

Mkutano wa Kimataifa wa Kuijenga Upya Iraq unatarajiwa kufanya Jumatatu ya tarehe 12 hadi Jumatano ya tarehe 14 mwezi huu wa Februari nchini Kuwait.

Serikali ya Waziri Mkuu wa Iraq, Haydar al Abadi, hivi karibuni iliandaa mpango maalumu wa kuyajenga upya maeneo yaliyoharibiwa vibaya na vita sambamba na kukarabiatiwa miundombinu ambayo iko katika hali mbaya kutokana na vita vya muda mrefu vya ndani ya Iraq.