Wahajiri wa Kiafrika walaani ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40839-wahajiri_wa_kiafrika_walaani_ubaguzi_wanaotendewa_na_utawala_wa_kizayuni
Maelfu ya wahajiri wa Kiafrika wameandamana mjini Tel Aviv kulaani ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Feb 25, 2018 04:04 UTC
  • Wahajiri wa Kiafrika walaani ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Kizayuni

Maelfu ya wahajiri wa Kiafrika wameandamana mjini Tel Aviv kulaani ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Waafrika hao waliandamana Jumamosi ambapo pia wamelaani sera ya utawala huo ya kuwarudisha makwao na kuwafunga jela wahajiri. Waandamanaji hao Waafrika walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "Sisi na Wanadamu",  huku wakilaani ubaguzi wa rangi katika utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumanne iliyopita wakuu wa utwala wa Kizayuni walipeleka kundi la kwanza la wakimbizi wa Eritrea katika jela ya Shahronim baada ya kuwashikilia kwa muda mrefu katika jela ya wazi ya Holot iliyo katika jangwa lenye joto kali.

Waafrika wakiandamana kupinga ubaguzi Tel Aviv

Mwezi Januari Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza kutekeleza mpango wa kuwatimua maelfu ya wahajiri wa Kiafrika walioingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu.

Israel ilidai kuwa imeafikiana na Rwanda na Uganda juu ya kuwakabidhi wahajiri hao kwa nchi hizo katika hatua ambayo imekosolewa vikali na watetezi wa haki za binadamu.