Wanachuo 340 wa Kipalestina wanashikiliwa katika magereza ya Israel
Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Palestina ametangaza kuuwa, kwa sasa wanachuo 340 wa Kipalestina wanashikiliwa katika magereza mbalimbali ya utawala haramu wa Israel.
Sabri Saidam amesisitiza kwamba, jeshi la utawala ghasibu wa Israel limeendelea kuvamia na kufanya hujuma katika maeneo ya elimu na kufanya vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wanafunzi na wanachuo wa Kipalestina.
Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Palestina amebainisha kwamba, jinai ya hivi karibuni kabisa ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wanachuo wa Kipalestina na uvamizi wake dhidi ya Chuo Kikuu cha Birzeit.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, jeshi la Israel lilifanyatua ovyo risasi katika hujuma yake hiyo na kumtia mbaroni Omar al-Keswani, Kiongozi wa Baraza la Wanachuo la Chuo Kikuu hicho.
Waziri Sabri Saidam ameeleza kuwa, hujuma na mashambulio ya jeshi la Israel dhidi ya Vyuo Vikuu vya Wapalestina ni ugaidi ulioratibiwa ambao haujawi kushuhudiwa hapo kabla.
Waziri huyo ameitaka Jumuiya ya Kimataifa ya Vyuo Vikuu na asasi za kimataifa kuchukua hatua za kukomesha uvamizi na miamala hiyo isiyo ya kibinadamu ya utawala ghasibu wa Israel.
Wakati huo huo, imeelezwa kuwa, zaidi ya wanawake 15, wametiwa mbaroni na utawala ghasibu wa Israel tangu mwaka 1967.
Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, takribani Wapalestina 7,000 wanashikiliwa katika magereza mbalimbali ya Israel na wanakabiliwa na mazingira mabaya kabisa.