Palestina yakaribisha maazimio ya UN dhidi ya utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i42190-palestina_yakaribisha_maazimio_ya_un_dhidi_ya_utawala_wa_kizayuni
Msemaji wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Palestina amekaribisha kupasishwa katika Umoja wa Mataifa maazimio matano ya haki za binadamu dhidi ya utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 25, 2018 23:49 UTC
  • Palestina yakaribisha maazimio ya UN dhidi ya utawala wa Kizayuni

Msemaji wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Palestina amekaribisha kupasishwa katika Umoja wa Mataifa maazimio matano ya haki za binadamu dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Yusuf al Mahmoud msemaji wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Palestina jana Jumapili alisema kuwa kupasishwa maazimio matano dhidi ya utawala wa Kizayunii katika Umoja wa Mataifa ni sababu ya kuwa na haki Wapalestina na ni dhihirisho la kuwa imara wananchi hao mbele ya dhulma, ukandamizaji, ukaliaji mabavu na kupinga kwao lugha ya mabavu na vitisho.  

Yusuf al Mahmoud amesema kuwa nchi zilizopasisha maazimio hayo zina misimamo na imani kubwa, ziko huru, zina heshima, na kusisitiza juu ya kuwepo usawa na uadilifu miongoni mwa walimwengu.  Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha Ijumaa iliyopita huko Geneva, zilipasisha kwa kura nyingi maazimio matano yaliyokuwa yamewasilishwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa  Kiislamu (OIC) kuhusu Palestina. 

Sisitizo kuhusu haki isiyopingika ya Palestina katika kujiainishia mustkablai na kuunda serikali huru, kurudi nyuma utawala wa Israel katika mipaka ya mwaka 1967 na kusitishwa uvamizi katika ardhi za Palestina, kuunga mkono haki za taifa la Palestina, kusitishwa ujenzi wa ukuta wa kibaguzi na kusimamishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ikiwemo huko Quds Mashariki na katika miinuko ya Golan, ni miongoni mwa masuala yaliyotajwa kwenye maazimio hayo.

Ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni huko al Quds 

Baada ya kupasishwa maazimio hayo, Nikki Haley Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alikasirishwa na hatua hiyo na kutishia kujiondoa katika baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni kulalamikia kupasishwa maazimio hayo dhidi ya utawala wa Kizayuni.