Kuzidi kulaaniwa Israel vamizi, upeo mpya kwa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44456-kuzidi_kulaaniwa_israel_vamizi_upeo_mpya_kwa_palestina
Wapenda haki duniani leo (Jumatatu) wameamua kufanya maandamano katika nchi 46 ulimwenguni ili kuilaani Israel suala ambalo limewafanya wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni washadidishe ulinzi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2018 02:13 UTC
  • Kuzidi kulaaniwa Israel vamizi, upeo mpya kwa Palestina

Wapenda haki duniani leo (Jumatatu) wameamua kufanya maandamano katika nchi 46 ulimwenguni ili kuilaani Israel suala ambalo limewafanya wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni washadidishe ulinzi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza.

Itakumbukwa kuwa, Jumatatu ya leo inasadifiana na tarehe 14 Mei, siku ya nakama kwa taifa la Palestina. Tarehe kama ya leo miaka 70 iliyopita yaani tarehe 14 Mei 1948 Milaadia, mabeberu na waistikbari wa dunia walitangaza rasmi kuundwa dola pandikizi la Israel katika kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu huko Palestina, na tangu wakati huo hadi hivi sasa, dondandugu hilo la kensa limekuwa likiumeng'enya kila kona mwili wa ulimwengu wa Kiislamu. Si hayo tu, lakini pia adui mwingine wa ulimwengu wa Kiislamu, rais wa hivi sasa Marekani, Donald Trump ameichagua siku ya leo kuuhamishia Quds ubalozi wa Marekani uliko Tel Aviv, mji mkuu wa utawala dhalimu wa Israel.

Mchoro unaoonesha ardhi za Waislamu za Palestina zilivyotekwa na kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni

 

Hata hivyo sambamba na wimbi kubwa la wapenda haki duniani kuamua leo kuutangazia ulimwengu uungaji mkono wao kwa malengo matakatifu wa Palestina, wananchi wa taifa hilo nao wameamua kujitokeza kwa wingi sana kutangaza upinzani wao kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Essam Bakr, mratibu wa makundi ya Palestina huko Ramallah amesema kuwa, wapenda haki ulimwengu, leo Jumatatu wameamua kufanya maandamano katika nchi 46 duniani kuiunga mkono Palestina na kulaani sherehe za kuhamishiwa Quds ubalozi wa Marekani uliko Tel Aviv. Wakati huo huo mamia ya maelfu ya Wapalestina wameamua kufanya maandamano leo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza ili kuungana na wapenda haki wengine duniani kumlaani Trump kwa uadui wake usio na kifani kwa taifa madhlumu la Palestina. Maandamano hayo ni muendelezo wa maandamano makubwa ya 'haki ya kurejea' yaliyoanza tarehe 31 Machi na kuendelea kila Ijumaa katika maeneo tofauti ya Palestina hususan karibu na mpaka wa Ghaza na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Shabaha kuu ya maandamano hayo ni kupigania kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi zao za asili na jadi. 

Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye hafichi chuki zake dhidi ya Waislamu wakiwemo Wapalestina

 

Kiujumla ni kwamba, kuongezeka wimbi la malalamiko ya wananchi dhidi ya uamuzi wa Donald Trump wa kuitangaza Quds yenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel, kumeamsha hisia za walimwengu ambao nao wameamua kuungana na Wapalestina kumsheheneza laana Trump na kuunga mkono malengo matakatifu wa Palestina. Uadui huo wa rais wa Marekani umepelekea kuanza Intifadha ya Tatu ya Wapalestina chini ya kaulimbiu ya "Muqawama, chaguo pekee la ukombozi wa Palestina na kukabiliana na njama dhidi ya Quds" ikiwa ni kaulimbiu inayoakisi waziwazi ujumbe na majibu ya wananchi wa Palestina kwa wavamizi wa Quds na waungaji mkono wao. 

Kiujumla ni kwamba matukio ya Palestina na mchakato wa mapambano ya Wapalestina ambao umeweza kuamsha hisia za walimwengu na kuwafanya wajitokeze kwa wingi sana kuyaunga mkono malengo matakatifu ya Palestina, ni ushahidi wa wazi kwamba chaguo la muqawama ndiyo njia pekee ya kuweza kukomboa ardhi za Palestina. Vile vile jambo hilo limeonesha kufeli Israel na muungaji mkono wake mkuu yaani Marekani ambao wamekuwa wakitumia kedi na hila tofauti kama vile kueneza fitna katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwagombanisha Waislamu wenyewe kwa wenywe ili kuisahaulisha kadhia ya Palestina. Vikao mbalimbali vya kieneo na kimataifa vya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na harakati mbalimbali za kuonesha kwa mifano uungaji mkono wa walimwengu kwa taifa la Palestina katika janibu tofauti za dunia, ni ushahidi mwingine wa wa wazi wa kufeli njama za kuisahaulisha na kuifuta kadhia ya Palestina.