NATO: Hatutaipa himaya Israel iwapo itashambuliwa na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45342-nato_hatutaipa_himaya_israel_iwapo_itashambuliwa_na_iran
Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) umesema hautaupa himaya utawala haramu wa Israel iwapo utashambuliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 03, 2018 07:24 UTC
  • NATO: Hatutaipa himaya Israel iwapo itashambuliwa na Iran

Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) umesema hautaupa himaya utawala haramu wa Israel iwapo utashambuliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ameliambia jarida la Ujerumani la Der Spiegel kuwa Israel ni mshirika lakini sio mwanachama wa muungano huo na kwa msingi huo utawala huo hauwezi kustafidi na dhamana ya usalama ya NATO.

Amesema shirika hilo la kujihami la kijeshi la NATO halijawahi kujihusisha na ima jitihada za amani au migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.

Wanajeshi wa nchi wanachama wa NATO

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitoa vitisho hewa mara kwa mara vya kuishambulia kijeshi Iran, lakini Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kuwa, uvamuzi au chokochoko zozote za utawala huo pandikizi zitakabiliwa kwa jibu kali.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala huo wa Kizayuni umekuwa ukiziasa Marekani na nchi za Ulaya kuachana na mkondo wa diplomasia na Iran haswa kuhusu miradi yake ya nyuklia, na badala yake umekuwa ukizitaka ziuunge mkono hatua za kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.