Jul 25, 2018 13:47 UTC
  • Moscow: Operesheni za Marekani huko Syria ni kinyume cha sheria

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa wanajeshi wa Marekani hawana haki yoyote ya kisheria ya kuendesha oparesheni zaidi huko Syria.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa, Marekani inaweza kubakia huko Syria kwa sharti kwamba ishirikiane na Moscow na Damascus katika suala la kurejea nyumbani wakimbizi wa Syria. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Igor Konashenkov ameeleza kuwa hakuna msingi wowote wa kisheria wa kuwahalalisha operesheni zaidi za wanajeshi wa Marekani  nchini Syria.   

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetoa maelezo hayo ikijibu matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Joseph Wottelr, kamanda wa kituo kikuu cha jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati. Hivi karibuni kamanda huyo wa majeshi ya Marekani alipinga suala la kushirikiana Marekani na Russia katika kurejea nyumbani wakimbizi wa Syria akisema  Moscow inaiunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. 

Rais Bashar al Assad wa Syria 

Jeshi la Marekani linafanya oparesheni za kijeshi huko Syria tangu mwaka 2014 bila ya idhini ya Damascus au kibali cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.  

Zoezi la kurejea nyumbani wakimbizi wa Syria kutoka katika mpaka wa Lebanon limenza kwa muda sasa ingawa Marekani na waungaji wake mkono wanajaribu kuzusha hofu na kuwatisha raia hao ili kuchelewesha na kukwamishwa zoezi hilo. Pamoja na vizuizi vyote hivyo, mamia ya raia wa Syria wamekwisharejea nchini hadi sasa kufuatia jitihada na uratibu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon. 

Tags