Wapalestina walaani Israel kumkamata Imam wa Masjid Al Aqsa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4747-wapalestina_walaani_israel_kumkamata_imam_wa_masjid_al_aqsa
Wapalestina wameendelea kulaani vikali hatua ya wanajeshi wa Israel kumkamata Imam na Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2016 22:35 UTC
  • Wapalestina walaani Israel kumkamata Imam wa Masjid Al Aqsa

Wapalestina wameendelea kulaani vikali hatua ya wanajeshi wa Israel kumkamata Imam na Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Katika taarifa yao ya pamoja ya jana Jumamosi, Kamati Kuu ya Waislamu wa Palestina, Baraza la Awqaf Palestina na taasisi nyingine za Kipalestina katika Quds Tukufu zimelaani wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kwa kumkamata Sheikh Mohamed Salim. Taarifa hiyo imesema hatua ya kumtia mbaroni Sheikh Salim siku ya Ijumaa ni hatari ambayo haijawahi kushuhudiwa. Taasisi hizo zimesema, hatua hiyo ya Israel inakusudia kubana uhuru wa kujieleza.

Aidha taasisi hizo za Kipalestina zimesema, kukamatwa Sheikh Mohammad Salim ni uingiliaji wa masuala ya kidini ya Waislamu na kusisitiza kwamba, "utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuchukua udhibiti kamili wa Masjid Al Aqsa ."

Siku ya Ijumaa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walimkamata Sheikh Mohammad Salim, Khatibu na Imamu wa Msikiti wa Al Aqsa baada ya sala ya Ijumaa. Katika hotuba zake za Ijumaa, Sheikh Salim alitoa wito kwa Wapalestina kuamka na kujitayarisha kukabiliana na hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuendelea kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa. Utawala wa Kizayuni unafanya njama za kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu na sehemu ya tatu kwa utukufu miongoni mwa Waislamu dunaini.