Aug 29, 2018 04:35 UTC
  • Radiamali ya Russia kwa njama mpya za Marekani dhidi ya Syria

Russia imeonya kuhusu taathira za njama na hatua zozote za kijeshi zitakazochukuliwa na Marekani na waitifaki wake dhidi ya Syria.

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameonya kuhusu njama mpya dhidi ya Syria na kueleza kuwa mashambulizi yoyote yatakayotekelezwa na Marekani dhidi ya Syria bila ya kuwasilisha hoja na ushahidi kwamba nchi hiyo imetumia silaha za kemikali yanatishia kupatiwa ufumbuzi kamili wa hali ya mambo. Makelele mapya ya kuituhumu Syria kwamba imetumia silaha za kemikali yalianza kusikika tangu Agosti 22 mwaka huu.  

Marekani, Uingereza na Ufaransa tarehe 22 mwezi huu wa Agosti zilitoa taarifa ya pamoja na kwa mara nyingine tena kuituhumu Syria kuwa imetumia silaha za kemikali. Nchi hizo aidha zilitahadharisha kuwa zitatoa jibu linalofaa kwa Damascus iwapo kutakaririwa mashambulio hayo ya kemikali yanayodaiwa kufanywa na serikali ya Damascus. Kuhusiana na suala hilo duru za Russia Ijumaa iliyopita ziliarifu kuwa kundi la watu wanaovalia kofia nyeupe wenye mfungamano na mashirika ya ujasusi ya Uingereza na Marekani wamepeleka katika mji wa Jisr- ash Shugur mkoani Idlib Syria mapipa manane ya gesi ya chlorine katika kutekeleza njama mpya dhidi ya Syria. 

Kundi la wanaovalia kofia nyeupe huko Syria 

Taarifa ya karibuni ya Marekani, Uingereza na Ufaransa na zile zilizohusiana na kundi hilo linalovalia kofia nyeupe zinaashiria uhakika huu kuwa Marekani na waitifaki wake hao zinatekeleza njama mpya dhidi ya serikali ya Syria kwa kisingizio cha kutumika silaha za kemikali.   

Tags