Ahmad Bahar: Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina
(last modified Sat, 06 Oct 2018 15:26:44 GMT )
Oct 06, 2018 15:26 UTC
  • Ahmad Bahar: Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina

Naibu Spika wa Bunge la Palestina amesema kuwa, hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel haiwezi kubadilisha ukweli wa mambo kwani Quds utaendelea kubakia kuwa mji mkuu wa daima wa Palestina.

Ahmad Bahar amesema kuwa, jeshi la Israel daima limekuwa likipiga makelele na kuuogopa muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina.

Naibu Spika wa Bunge la Palestina amesisitiza kuwa, maandamano ya 'Haki ya Kurejea' yataendelea hadi pale mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza utakapovunjwa kikamilifu.

Kadhalika kiongozi huyo wa Bunge la Palestina ameongeza kuwa, kushindwa mzingiro wa Gaza ni katika malengo ya Wapalestina na wananchi hao madhulumu wataendelea kutetea malengo yao.

Watoaji huduma za tiba pia hawasalimiki na jinai za askari wa utawala haramu wa Israel

Katika upande mwingine, Naibu Spika wa Bunge la Palestina amesema bayana kwamba, umoja na irada ya Wapalestina itaendelea kuweko hadi pale mzingiro wa Gaza utakapovunjwa kikamilifu na kuwasambaratisha wavamizi.

Aidha amesema kuwa, licha ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuitelekeza Palestina, lakini Wapalestina wataendelea na jihadi na muqawama wao na katu hawatishiki na vitisho vyay wavamizi.

Tangu tarehe 30 Machi mwaka huu hadi sasa, Ijumaa ya kila wiki, maelfu ya Wapalestina hushiriki kwenye maandamano ya Haki ya Kurejea ili kuonyesha upinzani wao kwa uvamizi na ukaliaji wa mabavu wa ardhi zao unaofanywa na Wazayuni pamoja na sera zao dhidi ya taifa la Palestina. Askari wa Kizayuni wanawashambulia moja kwa moja kwa risasi moto waandamanaji hao wasio na ulinzi na kuwaua shahidi au kuwajeruhi kadhaa miongoni mwao.

Tags