Katibu Mkuu wa Jihad al-Islami auonya utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48624-katibu_mkuu_wa_jihad_al_islami_auonya_utawala_haramu_wa_israel
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina ameonya kwamba, mapambano na muqawama una uwezo wa kuvifanya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko jirani na Ghaza visiwe kukalika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2018 22:57 UTC
  • Katibu Mkuu wa Jihad al-Islami auonya utawala haramu wa Israel

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina ameonya kwamba, mapambano na muqawama una uwezo wa kuvifanya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko jirani na Ghaza visiwe kukalika.

Ziad al-Nakhala amesisitiza kuwa, hujuma na mashambulio ya wanajeshi wa Israel dhidi ya maandamano makubwa ya 'Haki ya Kurejea' na kuwaua Wapalestina yanapaswa kusimamishwa.

Ziad al-Nakhala ambaye alichaguliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Jihad al-Islami akimrithi Dakta Ramadhan Abdullah Shalah amesema kuwa, muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina yatatoa jibu kwa wakati wake dhidi ya jinai za adui.

Maandamano ya Wapalestina ya "Haki ya Kurejea"

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Jihad al-Islami amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa mapambano na muqawama wa wananchi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kubainisha kwamba, usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza kkatu hauwezi kuufunga mikono muqawama na hivyuo uache kutetea taifa lake.

Aidha ameongeza kuwa, katu muqawama wa Palestina hautatia saini makubaliano yoyote yale ya kisiasa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao ni adui9 wa taifa la Palestina. 

Kadhalika Ziad al-Nakhala ametaka kuweko na umoja na mshikamano imara baina ya Wapalestina kwa shabaha ya kukabiliana na njama zenye lengo la kuliangamiza taifa la Palestina na kusisitiza kwamba, katu Marekani haiwezi kuwa rafiki wa taifa la Palestina au rafiki wa nchi za Kiislamu na Kiarabu.