Yemen yazitahadharisha nchi za Kiarabu zinazouhami utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128940-yemen_yazitahadharisha_nchi_za_kiarabu_zinazouhami_utawala_wa_kizayuni
Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameyatahadharisha makampuni ya meli kuhusu kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2025-07-30T12:37:50+00:00 )
Jul 30, 2025 12:37 UTC
  • Yemen yazitahadharisha nchi za Kiarabu zinazouhami utawala wa Kizayuni

Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameyatahadharisha makampuni ya meli kuhusu kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hazam al Assad amesema, awamu ya nne ya oparesheni ya majini ya Jeshi la Yemen ya kuwaunga mkono na kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza itatekelezwa dhidi ya makampuni yote ya meli ambayo yanashirikiana na bandari za utawala wa Kizayuni; sawa yawe ya nchi za Kiarabu au nchi nyingine. 

Al Assad ameongeza kuwa: Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimedhamiria kupanua oparesheni zake za kijeshi dhidi ya adui Mzayuni na waungaji mkono wake ambao wanashiriki katika mauaji na kuwazingira wananchi wa Gaza. 

Mwakilishi huyo wa ngazi ya juu wa harakati ya Ansrullah ya Yemen amesema: Ni doa la aibu kushiriki baadhi ya serikali za Kiarabu na Kiislamu katika mzingiro dhidi ya watu wa Gaza.