Russia: Tunataraji Marekani itatumia akili na busara kuhusiana na kadhia ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136290-russia_tunataraji_marekani_itatumia_akili_na_busara_kuhusiana_na_kadhia_ya_iran
Vassily Nebenzya, mwakilishi wa kudumu Russia katika Umoja wa Mataifa amesem kuwa, Moscow inatumai kwamba Marekani itatumia akili na busara kuhusiana na kadhia ya Iran.
(last modified 2026-02-06T02:32:06+00:00 )
Feb 05, 2026 11:41 UTC
  • Russia: Tunataraji Marekani itatumia akili na busara kuhusiana na kadhia ya Iran
    Russia: Tunataraji Marekani itatumia akili na busara kuhusiana na kadhia ya Iran

Vassily Nebenzya, mwakilishi wa kudumu Russia katika Umoja wa Mataifa amesem kuwa, Moscow inatumai kwamba Marekani itatumia akili na busara kuhusiana na kadhia ya Iran.

Nebenzya ameeleza kuwa, maamuzi ya hatua ya kijeshi dhidi ya Iran hayakubaliki na ni hatari.

Mwakilishi wa kudumu Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba, nchi yake inatarajia kwamba, viongozi wa Marekani watatumia busara na akili na kuachana na fikra ya kutaka kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran.

Mnamo Januari 28, Rais wa Marekani Donald Trump alianzisha tena vitisho vyake dhidi ya Iran ambapo sambamba na kuashiria uwepo wa meli ya kubeba ndege ya Abraham Lincoln katika maji ya eneo hilo, na kutangaza: "Meli kubwa inaelekea Iran."

Amir Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, pia alisema katika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama, akizungumzia vitisho vya Rais wa Marekani: "Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakataa na kulaani kauli hizo zinazochochea vita, ambazo hazina uwajibikaji na ni kinyume kabisa na kanuni za msingi za sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa."

Katika muhula wa pili wa urais wa Donald Trump, sera ya Marekani ya pande mbili kuelekea Iran imeonekana zaidi. Sera hii ni mchanganyiko wa vitisho vya kijeshi na shinikizo la kiuchumi kwa upande mmoja na mwaliko wa kujadiliana kwa upande mwingine, bila shaka, kwa lengo la Washington kufikia malengo inayotaka kutoka Tehran.