UNRWA: Watu wa Gaza wanazirai mitaani kwa sababu ya njaa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza leo Ijumaa kwamba Ukanda wa Gaza unasumbuliwa na hali mbaya na kwamba njaa imekithiri katika eneo hilo, na watu wanazimia barabarani kutokana na njaa kali.
UNRWA imetahadharisha kwa mara nyingine kuhusu hali ya mgogoro wa binadamu katika Ukanda wa Gaza na uhaba mkubwa bidhaa za chakula.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa: "Kila kitu kinakaribia kuisha kwa watu wa Ukanda wa Gaza huku kukiwa na ukosefu wa chakula, dawa za matibabu na maeneo salama kwa ajili ya hifadhi."
Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imenukuu ripoti ya UNRWA na kutangaza kuwa, mfumo wa kusambaza misaada wa sasa huko Gaza unaamiliana kinyume na ubinadamu na familia zenye njaa na hofu, zilizojeruhia na zilizochoka za Wapalestina.
Shirika la UNRWA limeeleza kuwa kuna mgogoro mkubwa wa njaa na ukosefu wa chakula katika Ukanda wa Gaza na kwamba wakazi wa eneo hilo wanazimia mitaani kutokana na njaa inayoongezeka.