Waziri Mzayuni ataka kubomolewa nyumba za viongozi wa HAMAS
(last modified Sun, 21 Oct 2018 07:43:48 GMT )
Oct 21, 2018 07:43 UTC
  • Waziri Mzayuni ataka kubomolewa nyumba za viongozi wa HAMAS

Yisrael Katz, Waziri wa Usafiri wa utawala haramu wa Israel ametoa wito wa kubomolewa nyumba za viongozi wa Harakati ya Mapambano ya kiislamu ya Palestina (HAMAS).

Matamshi hayo ya Yisrael Katz yanaonekana ni kuingiwa kiwewe na hofu viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ya kukabiliwa na mashambulio ya ulipizazi kisasi ya wanamapambano wa Kipalestina.

Yisrael Katz, Waziri wa Usafiri wa utawala haramu wa Israel ametishia kwamba, hatua yoyote ile ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa maeneo ya Naqab na Ghilaf huko Gaza itakabiliwa na kubomolewa nyumba moja baada ya nyingine za viongozi wa Hamas.

Aidha waziri akionekana kukweka ukosoaji wa kimataifa kuhusiana na mzingiro wa kila upande dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza amedai kwamba, Israel haitabeba dhima ya maafa ya eneo hilo.

UKosefu wa dawa Gaza kutokana na kuzingirwa eneo hilo

Ehud Barack, aliyewahi kushika nyadhifa za Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa utawala bandia wa Israel alikiri Ijumaa iliyopita kwamba, katika kipindi cha dakika 3 na sekunde thelathini aliowaua kwa umati Wapalestina 300.

Utawala wa Kizayuni  wa Israel umeliweka eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina chini ya mzingiro wa nchi kavu, anga na baharini kwa zaidi ya muongo mmoja sasa; hatua iliyowasababisha matatizo chungu nzima wakazi wa eneo hilo na kuwafanya wakabiliwe na maafa ya kutisha ya kibinadamu.  

Tags