Wanamapambano wa Palestina wajibu mapigo, vituo vya Wazayuni vyamiminiwa makombora
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49493-wanamapambano_wa_palestina_wajibu_mapigo_vituo_vya_wazayuni_vyamiminiwa_makombora
Harakati za mapambano za Palestina alfajiri ya Jumatatu zilijibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuvishambulia kwa makombora vitongoji zaidi ya 50 vya walowezi wa Kizayuni na vituo kadhaa vya askari wa Israel.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 13, 2018 23:07 UTC
  • Wanamapambano wa Palestina wajibu mapigo, vituo vya Wazayuni vyamiminiwa makombora

Harakati za mapambano za Palestina alfajiri ya Jumatatu zilijibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuvishambulia kwa makombora vitongoji zaidi ya 50 vya walowezi wa Kizayuni na vituo kadhaa vya askari wa Israel.

Duru za habari zinasema kuwa, hadi sasa zaidi ya makombora na maroketi 400 yamevurumishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Mashambulizi hayo ya harakati za mapambano ya ukombozi za Palestina ni jibu kwa jinai na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita. Miji na maeneo mengi ya Israel yalijawa na sauti za ving'ora vya tahadhari, na Wazayuni walionekana wakikimbia huku na kule kutafuta pa kujikinga na makombora na wanaharakati wa Palestina. Awali makundi ya mapambano ya Palestina yalikuwa yametangaza kuwa, yatajibu mashambulizi ya aina yoyote ya Israel kwa mujibu wa kanuni ya kulipiza kisasi na wajibu wa kujihami. 

Basi la askari wa Israel lililolengwa kwa kombora la wanaharakati wa Paletina.

Hali ya sasa ya Palestina inaonesha kuwa, harakati za mapambano za Palestina zimevuka kipindi cha kusubiri kushambuliwa na kujibu mapigo tu na sasa harakati hizo zinalenga maeneo muhimu ya Wazayuni na kuzusha mlingano wa hufo. Awamu hii ya mapambano ya Wapalestina ni sehemu ya Intifadha mpya ya kukabiliana na njama za Marekani na Israel dhidi ya Quds tukufu na harakati zao za kutaka kukanyaga haki zote za Wapalestina kupitia mpango wa unaosimamiwa na Donald Trump wa "Muamala wa Karne". 

Jibu la mamia ya makombora na maroketi ya Wapalestina dhidi ya uchokozi wa Israel ni sawa na kutunisha misuli harakati za mapambano za Ukanda wa Gaza mbele ya utawala ghasibu wa Tel Aviv. Harakati hizo sasa zinatumia stratejia ya "mashambulizi dhidi ya mashambulizi. Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umeshindwa kufikia malengo yake katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na huko Syria, sasa unafanya njama za kutaka kuficha na kufunika kufeli huko kwa kutunisha misuli na kuua raia wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. Jinai hizo zimejibiwa na wanamapambano wa Palestina kwa kuvurumusha mamia ya makombora na maroketi dhidi ya vituo vya sakari wa Kizayuni na vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Wanaharakati wa Kiislamu wa Palestina wakijitayarisha kuvurumisha makombora dhidi ya Israel.

Kwa sasa Marekani, Israel na Saudi Arabia zinafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kuulinda utawala huo ghasibu kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutaka kuhuisha eti mapatano ya Wapalestina na Israel. Harakati hizo zilishika kasi kubwa zaidi baada ya Donald Trump kushika hatamu za uongozi huko Marekani na kiongozi huyo anashirikiana na baadhi ya tawala za Kiarabu hususan Saudi Arabia kwa ajili ya kukanyaga kikamilifu haki za taifa la Palestina kupitia njama kadhaa kama ile ya "Muamala wa Karne" na kujenga uhusiano rasmi wa kidiplomasia baina ya nchi za Kiarabu na utawala ghasibu unaoikalia Quds kwa mabavu. Hata hivyo wanaharakati wa Palestina waling'amua mapema njama hizo za Marekani, Israel na Saudi Arabia na kujibu mapigo kwa mbinu mpya na za aina yake.

Maandamano ya wakazi wa Gaza dhidi ya Israel.

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" yanayofanywa kila siku ya Ijumaa na watu wa Ukanda wa Gaza na majibu ya maroketi na makombora ya harakati za mapambano ya Kiislamu dhidi ya Israel ni sehemu ya jitihada za Wapalestina za kuzima na kufubaza mipango ya kishetani ya Israel na washirika wake.