Syria yatungua makombora ya Israel yaliyoelekezwa Damascus
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50814-syria_yatungua_makombora_ya_israel_yaliyoelekezwa_damascus
Jeshi la Syria limetoa jibu kali kwa uvamizi mpya wa Israel, baada ya utawala huo wa Kizayuni kuanzisha mashambulizi ya makombora viungani mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 12, 2019 04:16 UTC
  • Syria yatungua makombora ya Israel yaliyoelekezwa Damascus

Jeshi la Syria limetoa jibu kali kwa uvamizi mpya wa Israel, baada ya utawala huo wa Kizayuni kuanzisha mashambulizi ya makombora viungani mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi hiyo umetungua makombora hayo ya Israel, yaliyovurumishwa kutoka eneo la Galilee kuelekea Damascus usiku wa kuamkia leo.

SANA pia imemnukuu ofisa mmoja wa Wizara ya Uchukuzi Syria ambaye hakutaka jina lake litajwe akisema kuwa, chokochoko hiyo ya Wazayuni haijaathiri kivyovyote shughuli katikia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Damascus.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala haramu wa Israel umekuwa ukitekeleza mashambulizi yanayolenga vituo vya kijeshi vya Syria, kwa kisingizio cha kupambana na magenge ya kigaidi, lakini umekuwa ukikabiliwa na jibu kali.

Kutunguliwa makombora ya Wazayuni

Lengo la mashambulizi hayo ya kivamizi ya Israel ndani ya ardhi ya Syria ni kuyalinda magenge ya kigaidi na ya ukufurishaji kama vile Daesh (ISIS) na Jabhat al Nusra, ambayo yanaelekea kusambaratishwa kikamilifu.

Mbali na Tel Aviv kuyapa silaha makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali halali ya Damascus, lakini pia imekuwa ikiwapa matibabu matakfiri waliojeruhiwa nchini Syria.