Hamas yataka kususiwa sarafu dola ya Marekani
(last modified Fri, 19 Jul 2019 02:33:11 GMT )
Jul 19, 2019 02:33 UTC
  • Hamas yataka kususiwa sarafu dola ya Marekani

Musa Abu Marzouq mjumbe wa ngazi ya juu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa wito wa kususiwa sarafu ya dola ya Marekani.

Akizungumza na vyombo vya habari, Abu Marzouq amezitolea wito nchi zote kususia sarafu ya dola ya Marekani na kuacha kuitumia katika miamala yao ya biashara ili kuzuia kuimarika uchumi wa Marekani ambayo imeamua kuanzisha vita vya kibiashara dhidi ya nchi nyingine. 

Musa Abu Marzouq, Mwakilishi wa ngazi ya juu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas 

Mjumbe huyo wa ngazi ya juu wa Hamas amesisitiza kuwa serikali ya Marekani imewawekea vikwazo watu milioni 80 nchini Iran; hatua ambayo ni kinyume cha sheria kwa sababu ni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pekee ndilo lenye mamlaka ya kuziwekea vikwazo nchi mblimbali. 

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 8 Mei mwaka jana aliiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na hivyo kukiuka majukumu y Washington kuhusiana na makubaliano hayo ya kimataifa. Baada ya kuchukua uamuzi huo wa upande mmoja, Trump alianza tena kutekeleza vikwazo vya nchi yake dhidi ya Iran. 

Tags