Hizbullah: Marekani haijapata natija yoyote katika mapambano yake dhidi ya muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55036-hizbullah_marekani_haijapata_natija_yoyote_katika_mapambano_yake_dhidi_ya_muqawama
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji katika Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesisitiza kwamba mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani dhidi ya muqawama, yalikuwa na lengo la kufanya muqawama huo uachane na majukumu yake ya kuilinda Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 27, 2019 23:56 UTC
  • Hizbullah: Marekani haijapata natija yoyote katika mapambano yake dhidi ya muqawama

Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji katika Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesisitiza kwamba mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani dhidi ya muqawama, yalikuwa na lengo la kufanya muqawama huo uachane na majukumu yake ya kuilinda Lebanon.

Sheikh Ali Damush ameongeza kwamba lengo la serikali ya Washington la kuuwekea muqawama mashinikizo ya kiuchumi, kifedha na vikwazo, lililenga kuufanya usalimu amri na kuachana na majukumu yake ya kuilinda Lebanon pamoja na  kutofuatilia haki ya maji na mafuta ya nchi hiyo ambavyo vinakodolewa macho na utawala haramu wa Kizayuni.

Sheikh Ali Damush, Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji katika Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon

Sheikh Ali Damush  ameashiria uadui uliopo dhidi ya muqawama ukiongozwa na Marekani na kubainisha kwamba baada ya Washington kukata tamaa ya kuibua vita vya kijeshi na pia kufeli katika kueneza propaganda chafu dhidi ya Harakati ya Hizbullah sambamba na kushindwa kupata natija katika kuiweka harakati hiyo kwenye orodha inayoitwa eti ya kigaidi, imeamua kutumia stratijia ya vikwazo na vita vya kiuchumi dhidi ya harakati hiyo ya Kiislamu. Aidha Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesisitiza kwamba siasa za vikwazo pia zitafeli kupitia stratijia ya kusimama imara, subira, irada thabiti na azma ya dhati ya muqawama. Amezidi kubainisha kwamba Lebanon si tu kwamba ni eneo lisilofaa kwa ajili ya kutekelezwa siasa za Marekani dhidi ya muqawama, bali ni uwanja wa ushindi wa muqawama huo.